Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 102 2025-02-04

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Nyumba za Polisi kwenye Kituo cha Polisi Micheweni?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatarajia kutenga fedha kiasi cha shilingi 368,770,600/= toka kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2025/2026, kwa ajili ya kujenga nyumba mbili za makazi ya kuishi familia sita za Askari Polisi katika Kituo cha Polisi Micheweni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi 802,926,788/= kwa ajili ya kujenga kituo kipya cha Polisi daraja “B” cha Micheweni, kwani kituo kilichopo sasa ni kichakavu na hakiwezi kufanyiwa ukarabati. Ujenzi huo unatarajia kuanza katika mwaka wa fedha 2024/2025, ahsante.