Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omar Issa Kombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wingwi
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Nyumba za Polisi kwenye Kituo cha Polisi Micheweni?
Supplementary Question 1
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini kwa kuwa ni muda mrefu nimeuliza maswali kuhusu ujenzi wa Kituo cha Polisi pamoja na nyumba za Askari, na Mheshimiwa Waziri ametuambia kwamba, ametenga shilingi 800,000,000/=, sasa je, ni quarter gani ya mwaka wa fedha ujenzi huu wa Kituo cha Polisi Micheweni utaanza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri uko tayari kupanga ratiba yako baada ya Mkutano huu wa Bunge, kuambatana nami kwenda kutembelea Kituo hiki cha Polisi Micheweni?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, fedha imetengwa kwenye mwaka wa fedha 2024. Kwa hiyo, kwenye quarter hii ya tatu na ya nne itatolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha Polisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utayari wa Kwenda huko baada ya Bunge lako Tukufu; nitakaa na Mheshimiwa Mbunge, tutapanga ratiba ya kwenda kutembelea Kituo hicho cha Micheweni, ahsante.
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Nyumba za Polisi kwenye Kituo cha Polisi Micheweni?
Supplementary Question 2
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumwuliza swali Mheshimiwa Naibu Waziri. Tuliomba fedha za ukarabati wa Vituo vya Polisi Kwamtoro pamoja na Mrijo na tuliahidiwa mwaka huu wa fedha wangetoa hiyo fedha, lakini mpaka sasa fedha haijaenda. Ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ukarabati wa vituo viwili vya Polisi; Kwamtoro pamoja na Mrijo, Wilayani Chemba?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama tulivyosema katika mwaka wa fedha 2024/2025 tutapeleka fedha, kwa kuwa mwaka bado unaendelea. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge asiwe na wasiwasi fedha itakuja kwa ajili ya ukarabati wa vituo viwili vya Polisi vya Chemba, ahsante.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Nyumba za Polisi kwenye Kituo cha Polisi Micheweni?
Supplementary Question 3
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kituo cha Polisi cha Mgeta, Serikali imetoa shilingi 53,000,000/= na sasa ghafla kimesimama, hakiendelei kujengwa. Ni lini sasa kituo hicho kitamalizika?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumeshatoa fedha kiasi cha shilingi 53,000,000/=, basi namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, baada ya kipindi cha maswali, nitakutananaye. Tutafuatilia ni kwa nini kituo hicho kisikamilike wakati fedha imetolewa? Ahsante
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved