Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 129 2025-02-06

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:-

Je, Serikali inachukua hatua gani kwa Maafisa Masuuli na Wahazini wa Serikali za Mitaa kutokana na ongezeko la hoja za ukaguzi za Ripoti za CAG?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Taarifa za CAG zinaonesha kuwa, mwenendo wa hati za ukaguzi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka. Katika kipindi cha miaka minne (2019/2020 hadi 2022/2023), Hati Safi zimeongezeka kutoka 124 sawa na 67% mwaka 2019/2020 hadi Hati 181 sawa na 98.4% mwaka 2022/2023. Aidha, hati zenye shaka na hati mbaya zimepungua kutoka 61 sawa na 33% mwaka 2019/2020 hadi Hati tatu sawa na 1.6% mwaka 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, mwenendo huu mzuri wa Hati za Ukaguzi na utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi umechangiwa na uchukuaji wa hatua za kisheria na kinidhamu kwa watumishi wanaosababisha hoja za ukaguzi au hasara kutokana na kutotekeleza wajibu wao kikamilifu au kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu.

Mheshimiwa Spika, mathalani, kufuatia Taarifa ya CAG ya ukaguzi wa Mwaka wa Fedha 2022/2023, jumla ya watumishi 294, wakiwemo Wakurugenzi na Waweka Hazina, wamechukuliwa hatua mbalimbali zikiwemo kufukuzwa kazi (20), kifungo jela (watano), kufikishwa Mahakamani (30), kushushwa cheo (mmoja), kupewa onyo (100), kukatwa mshahara (14) na kufikishwa Polisi na TAKUKURU kwa uchunguzi (114).

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya udhibiti ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma na kupunguza hoja za ukaguzi na itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watakaokiuka taratibu zilizopo, ahsante.