Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 130 2025-02-06

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:-

Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uwepo wa vituo vya huduma ambavyo ni vikongwe na chakavu vinavyohitaji ukarabati. Ili kutekeleza jukumu hilo, Serikali ilifanya tathmini ya vituo chakavu, ambapo mpaka Disemba, 2024 kuna jumla ya vituo vya afya 204 na zahanati 1,226 zinazohitaji ukarabati kote nchini zikiwemo Zahanati za Sirop, Getanuwas na Dirma katika Wilaya ya Hanang’

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ukarabati wa vituo chakavu kwa awamu na mpango wa Serikali ni kuongeza kasi ya ukarabati wa vituo vya afya na zahanati mara baada ya kukamilisha ukarabati wa hospitali kongwe 77 ambapo tayari hospitali 14 zimekwisha karabatiwa na hospitali 34 ukarabati unaendelea ambapo jumla ya shilingi shilingi bilioni 44.5. Ahsante.