Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 1
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa majibu ya Serikali hospitali kongwe ambazo zimekwisha kukarabatiwa ni 18% tu. Kata ambazo Mheshimiwa Waziri amezitaja zina idadi kubwa ya watu na kweli ukiboresha huduma za afya za msingi maana yake hospitali zitapunguza kupokea watu na itakuwa rahisi watu kufikia huduma za afya.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Je, Serikali sasa haioni sasa kuna dharura ya kukarabati na kujenga nyumba za watumishi pamoja na huduma ya mama na mtoto kwenye Zahanati ya Dirma, Sirop, Ishponga na Getanuwas?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kituo cha Afya Hirbadaw kina upungufu mkubwa wa vifaatiba hasa jokofu la kuhifadhia maiti. Je, Serikali ina mkakati gani wa kupeleka vifaa vya kutosheleza kwenye Kituo cha Afya cha Hirbadaw?
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna baadhi ya vituo vya afya ambavyo ni chakavu na vina upungufu wa baadhi ya majengo yakiwemo majengo ya huduma ya afya ya mama, baba na mtoto.
Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba maeneo yote ambayo ya zahanati au vituo vya afya ambavyo havina majengo hayo Serikali imekuwa ikiweka kipaumbele kuhakikisha kwamba majengo hayo yanajengwa ili yaweze kutoa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, katika vituo vyake ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja katika Jimbo la Hanang tutahakikisha tunavifuatilia na kutafuta fedha aidha kupitia mapato ya ndani au Serikali Kuu ili majengo hayo ya huduma ya mama, baba na mtoto yaweze kujengwa na wananchi wapate huduma hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, kuhusiana na kituo cha afya ambacho Mheshimiwa Mbunge amekitaja ambacho hakina vifaatiba, ninaomba tu nimhakikishie kwamba Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha huu ameshapeleka katika halmashauri zote 184 kati ya shilingi milioni 800 mpaka shilingi bilioni tatu kwa kila halmashauri kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, natumia nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang kuweka kipaumbele cha vifaatiba kwenye kituo hicho cha afya ambacho hakina vifaatiba, lakini Serikali imekwishapeleka fedha
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Name
Robert Chacha Maboto
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda Mjini
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 2
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, je, Serikali itajenga lini Kituo cha Afya katika Kata ya Sazira na Kata ya Guta katika Halmashauri ya Mji wa Bunda? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka mpango mkakati wa ujenzi wa vituo vya afya kwenye kata za kimkakati ambazo zinakidhi vigezo vya idadi ya wananchi wasiopungua 15,000, lakini umbali kutoka kituo cha jirani zaidi lakini na hali za kijiografia.
Mheshimiwa Spika, nimwelekeze Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na Mkurugenzi na ninafahamu anashirikiana vizuri na alishaleta taarifa hiyo. Watuletee rasmi andiko la maombi ya vituo hivyo vya afya katika kata hizo ili Serikali iweke kwenye mpango kazi wa ujenzi wa vituo hivyo kwa kushirikiana na mapato ya ndani ya halmashauri. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 3
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. Mheshimiwa Naibu Waziri, unaonaje baada ya kumaliza Bunge hili uongozane nami kwenda Jimbo la Momba? Tupitie Kijiji cha Makamba, Kijiji cha Sanja, Siliwiti na Itumba ili uone changamoto ambayo wananchi wanapitia baada ya kukosa zahanati?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nipo tayari kuambatana na Mheshimiwa Mbunge kwenda katika Jimbo lake la Momba na katika vijiji ambavyo amevitaja ili tuweze kushirikiana kuona namna nzuri ya kujenga zahanati katika maeneo hayo. Wakati huo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sauti yake inasikika ipasavyo na tayari ameleta majina ya vijiji hivyo. Serikali iko kwenye utaratibu wa kutafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hizo. Ahsante sana.
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 4
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kituo cha Afya cha Moshono, Wilaya ya Arusha Mjini, kina nyufa nyingi na hasa kwenye jengo la mama na mtoto na hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi. Je, ni upi mkakati wa Serikali kukarabati kituo hiki?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninaomba kutumia nafasi hii kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwelekeza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha atume wataalam wake, wahandisi wa ujenzi, waende wakafanye tathmini ya jengo hilo lenye nyufa. Ikiwa ni hatarishi, basi hatua stahiki zichukuliwe mapema na Serikali iweke utaratibu wa kukarabati au kujenga jengo lingine, ili kuhakikisha kwamba, wananchi wanakuwa salama na wanapata huduma bora. Ahsante sana.
Name
Deo Kasenyenda Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makambako
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 5
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nini mpango wa Serikali kuunga mkono jitihada za wananchi wa Mkolango, ambao wamejenga? Wanaomba hela, Serikali imalizie nguvu zao. Nakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga amefuatilia kwa karibu sana suala la Zahanati ya Mkolango na ninafahamu wananchi walitoa nguvu zao, zaidi ya miaka saba wanasubiri Serikali kukamilisha. Ninaomba kumhakikishia, kama ambavyo tumekubaliana, tumeshaingiza kwenye vipaumbele vya mwaka huu wa fedha kupata fedha hiyo, kwa ajili ya kukamilisha Zahanati ya Mkolango. Ahsante sana.
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 6
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, vijiji vingi vya Mbogwe vilishajenga maboma ya zahanati. Mpango wa Serikali ukoje kutoa pesa, ili zahanati hizi ziweze kukamilika wananchi waendelee kupata huduma? Ninakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali hii ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tangu mwaka 2021 mpaka sasa zaidi ya shilingi 15,000,000,000 hadi shilingi 30,000,000,000 zinatolewa kila mwaka, kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati na vituo vya afya katika halmashauri zote, kote nchini, ikiwemo Halmashauri ya Mbogwe.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, nafahamu kwamba, kuna zahanati zimekamilishwa kwa fedha ya Serikali Kuu, lakini nafahamu bado kuna maboma, tuwapongeze wananchi kwa kazi hiyo nzuri. Nakuhakikishia kwamba, Serikali itaendelea kutenga fedha, kwa ajili ya kukamilisha maboma hayo katika Wilaya ya Mbogwe. Ahsante.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 7
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kituo cha Afya Iramba Ndogo kina jengo moja tu lililokamilika la OPD, hakuna jengo la wazazi, maabara na kichomea taka. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kujenga majengo hayo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ujenzi wa vituo vya afya unafanyika kwa awamu, tulianza na awamu ya kwanza ya majengo ya OPD, maabara na majengo mengine. Namhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge, tunafahamu kwamba, Kituo cha Afya cha Iramba Ndogo kina jengo moja na majengo mengine muhimu bado hayajajengwa.
Mheshimiwa Spika, kwa bahati nzuri tumekwishakiweka kwenye mpango wa ujenzi wa majengo yaliyobaki. Kwa hiyo, ninaomba kukuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali inalifanyia kazi suala hilo. Ahsante.
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 8
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa swali dogo la nyongeza. Hospitali ya Wilaya ya Kyela majengo yake yamechakaa sana, hata unapokwenda kuona wagonjwa unahisi huruma sana. Sasa je, ni lini Serikali itapeleka fedha za kujenga hospitali ile, angalau hata kwa kukarabati? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli Hospitali ya Wilaya ya Kyela ni hospitali kongwe, kwa bahati njema nimefanya pale kama miaka tisa, naifahamu vizuri sana. Serikali hii sikivu imeweka mpango madhubuti, ilishapeleka fedha, kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ghorofa, najua limeanza ujenzi na tumeweka mpango wa kujenga majengo yote ya wodi na OPD yawe bora zaidi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba kukuhakikishia kwamba, Serikali imeshaiingiza kwenye mpango na tutaendelea kujenga kwa awamu, ili kuibadilisha kabisa Hospitali ya Wilaya ya Kyela.
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 9
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, Zahanati ya Welu ambayo ipo katika Kata ya Ulanda, Jimbo la Kalenga, ambayo inahudumia vijiji vinne, imejengwa na imekarabatiwa vizuri, lakini ina changamoto ya daktari. Nini mkakati wa Serikali kupeleka daktari? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninaomba kutumia nafasi hii kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, kumsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhakikisha kwamba, wanafanya msawazo wa ndani kutoa mganga kutoka zahanati ambayo ina waganga zaidi ya wawili au watatu, ili wapelekwe pale, kwa ajili ya kuongeza huduma za afya kwenye Zahanati ya Welu.
Mheshimiwa Spika, wakati huo huo, ninamhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge, Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira na mwaka huu wa fedha wataalam zaidi ya 10,183 wamekwishaajiriwa na Wilaya ya Iringa itapata wataalam hao. Kwa hiyo, tutaendelea kuboresha ikama ya watumishi na ninamhakikishia tu kwamba, hicho ni kipaumbele cha Serikali. Ahsante.
Name
Iddi Kassim Iddi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 10
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, Zahanati ya Kijiji cha Kabondo, Kata ya Mwanase, ni muda sasa haijakamilika. Nataka kufahamu Kauli ya Serikali, ni lini sasa zahanati hii itakamilika na kuanza kutoa huduma, ili wananchi wa Kabondo waweze kupata huduma ya zahanati?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, katika ukarabati na ukamilishaji wa zahanati, ziko zahanati ambazo zilianza ujenzi kwa nguvu za wananchi, lakini Serikali ikapeleka shilingi 50,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji. Kwa hiyo, kwa zahanati ambazo zilipokea shilingi 50,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji zikiwa hatua ya lenta, tunatarajia ziwe zimekamilika na zimeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kuchukua nafasi hii kumuhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, zahanati hiyo ya Kabondo tutaifuatilia, kama ilipokea shilingi 50,000,000 basi inatakiwa iwe imekamilika na tutachukua hatua stahiki kuhakikisha kwamba, inakamilika kwa wakati, lakini kama haijapokea tutaiingiza kwenye kipaumbele cha zahanati ambazo zitaletewa fedha hiyo ili iweze kukamilika. Ahsante.
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 11
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi. Vijiji vya Makinda, Mitawa B, Nyera na Tepetepe vina uhitaji mkubwa sana wa ujenzi wa zahanati na wananchi wameshaanza. Je, Serikali iko tayari kuwa-support wananchi hawa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, vijiji vyote ambavyo vina mpango wa ujenzi wa zahanati na ambavyo wataalam wamejiridhisha kwamba, vinakidhi vigezo vya ujenzi wa zahanati tunawapongeza wananchi ambao wameanza kutoa nguvu zao, kwa ajili ya ujenzi huo.
Mheshimiwa Spika, nawahakikishia tu kwamba, Serikali kwa awamu itaendelea kutenga bajeti, kwa ajili ya kuchangia nguvu za wananchi na kukamilisha zahanati hizo katika Jimbo la Liwale, lakini pia, katika majimbo mengine katika nchi yetu kwa ujumla.
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 12
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali imefikia wapi mpango wa kuvikarabati Vituo vya Afya vya Lusewa, Mkongo Gulioni na Mputa, Wilayani Namtumbo, ambavyo vilijengwa miaka ya 70? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Vita Kawawa amewasilisha mara kadhaa hoja hiyo ya ukarabati wa Vituo hivyo vya Afya vya Mkongo na vingine. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika vile vituo vya afya 204 ambavyo vimefanyiwa tathmini na kwamba, ni vikongwe na vichakavu katika Jimbo la Namtumbo, vimo kwenye orodha hiyo. Kwa hiyo, naomba kumhakikishia tu kwamba, baada ya ukamilishaji wa ukarabati wa hospitali za wilaya tutahakikisha tunatoa kipaumbele kuanza ukarabati wa vituo hivyo vya afya, ahsante.
Name
Salma Rashid Kikwete
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mchinga
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 13
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itatupelekea pesa katika Zahanati yetu ya Mputwa na hasa, kwenye nyumba ya watumishi? Kwa sababu, nyumba ile ya watumishi imejengwa kidogo, upande huu kuna sitting room na chumba kimoja; sasa sitting room anakaa mtumishi mmoja na watoto wake halafu kwenye chumba anakaa mtumishi wa kiume.
Mheshimiwa Spika, ina maana kwamba, wanakaa sehemu moja, hata wakitaka kwenda kujisaidia ni shida, inabidi huyu apite hapa kwa kina mama halafu aende kule. Sasa, je, lini mtatupatia pesa kumalizia ile nyumba ya watumishi? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa, mama yangu, Salma Kikwete amelisema hili suala, ni suala nyeti na amekuwa akifuatilia sana ustawi wa wananchi wa Jimbo la Mchinga. Ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwanza dhamira ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wetu katika sekta ya afya wanakaa katika mazingira bora ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, kuna Mpango wa Serikali ambao unatekelezwa sasa, wa ujenzi wa nyumba za two in one na three in one na zoezi hili ni endelevu. Ninaomba kupokea hoja ya Mheshimiwa Mbunge, twende tukaifanyie kazi kwa haraka kupata fedha, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi katika zahanati ambayo ameitaja.
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 14
MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumuuliza swali Mheshimiwa Naibu Waziri juu ya fedha za Kituo cha Afya cha Chomachankola pamoja na Uswai. Je, ni lini fedha hizo mtatupatia? Ninakushukuru sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Chomachankola kimeingizwa kwenye mpango wa Benki ya Dunia (Team Chip) na tuko hatua za mwisho. Jana kulikuwa na kikao cha Ofisi ya Rais, TAMISEMI na watu wa World Bank kuweka mpango wa ku-release zile fedha, kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo. Kwa hiyo, ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Gulamali kwamba, tuko hatua za mwisho kutoa fedha hiyo, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Chomachankola. Ahsante.
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali wa kuboresha zahanati za zamani zilizopo Makao Makuu ya Kata za Hanang’?
Supplementary Question 15
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya, Ipogolo na Kituo cha Afya Ngome, ni vituo vikongwe sana vya miaka zaidi ya 30. Ni lini Serikali itatuletea, hasa, wodi za kisasa za kujifungulia wanawake?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, katika vituo vyetu vya afya, vipo vituo ambavyo ni vikongwe, lakini vina miundombinu yote na pia, vipo vituo vya afya ambavyo vina miundombinu pungufu na hususan wodi za wanawake, wanaume na watoto.
Mheshimiwa Spika, nafahamu vituo vya afya vikongwe na vingine ambavyo amevitaja Mheshimiwa Mbunge vina upungufu wa majengo hayo na tumeshaweka mpango wa awamu ya pili ya upanuzi na ukarabati.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nakuhakikishia Mheshimiwa Msambatavangu kwamba, Serikali itahakikisha inatenga fedha, inaweka kipaumbele, inakwenda kukarabati na kufanya upanuzi wa vituo hivyo vya afya. Ahsante sana.