Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 131 2025-02-06

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – (MHE. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kata ya Mabogini ina jumla ya shule za sekondari tatu ambazo ni Mpirani yenye jumla ya wanafunzi 1,158, Mabogini wanafunzi 711 na Mtakuja B wanafunzi 234. Aidha, Mwaka wa Fedha 2022/2023 Serikali ilipeleka shilingi milioni 584.2, kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kutwa katika Kata ya Mabogini. Ujenzi wa shule hii umekamilika na kusajiliwa kwa jina la Mtakuja B Sekondari.

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali kwa sasa ni kujenga shule za kutwa kwa kuzingatia vigezo vitatu ambavyo ni, kila kata kuwa na shule ya sekondari walau moja katika maeneo ya msongamono mkubwa wa wanafunzi na sehemu ambazo watoto wanatembea zaidi ya kilometa 5. Kwa kuzingatia kuwa, Kata ya Mabogini tayari ina shule tatu za sekondari, haijaingizwa kwenye mpango wa kujengewa shule nyingine ya sekondari. Ahsante.