Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?
Supplementary Question 1
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza. Kutoka Kijiji cha Mvuleni, Mji Mpya, mpaka kufika kwenye hiyo shule ya sekondari inayojengwa ni zaidi ya kilometa tano. Vigezo vinaonesha, zikishazidi kilometa tano ni lazima kuwe na shule na population katika kata ile ni zaidi ya watu 50,000. Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga shule nyingine, ili kuweza kuwapunguzia wanafunzi wetu makali?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kuna maeneo mengi nchini yenye urefu wa namna hiyo na watoto wetu wa kike wanaathirika kwa kupata mimba za utotoni. Je, Serikali haioni ni wakati sasa wa kufanya utafiti na kujenga shule ambazo ziko mbali zaidi ya kilometa tano ili kusaidia wanafunzi wetu? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, ziko kata ambazo zina idadi kubwa ya wananchi, lakini kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ametaja, Kata hiyo ya Mvuleni na Mji Mpya kwamba, zina umbali wa zaidi ya kilometa tano na wananchi zaidi ya 50,000.
Mheshimiwa Spika, naomba tulichukue suala hilo, ni suala muhimu, twende tukaone uwezekano wa kufanya tathmini na pia, uwezekano wa kupata fedha, kwa ajili ya kuboresha huduma za elimu katika eneo hilo na kupunguza umbali kwa wanafunzi. Kwa hiyo, Serikali hii sikivu tutahakikisha tunalifanyia kazi ili tuweze kutoa maamuzi bora zaidi.
Mheshimiwa Spika, pili, ni kweli kwamba, katika nchi yetu zipo baadhi ya kata ziko mbali zaidi, lakini sera ni ndani ya kilometa tano tunakuwa na shule ya sekondari ndani ya kata. Kwa hivyo, zile kata ambazo zina umbali mkubwa zaidi tunaendelea kufanya tathmini na kupeleka fedha, kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari, ikiwa vigezo vyote vitakuwa vimetimia. Ahsante.
Name
Michael Constantino Mwakamo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?
Supplementary Question 2
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Spika, ninafahamu kwamba, Serikali ina mpango wa kujenga shule za sekondari za kata nchi nzima katika kata ambazo hazipo. Je, Serikali ina mpango gani wa kutupatia pesa kujenga shule za Kata ya Janga na Mtambani, pale katika Mji Mdogo wa Mamlaka, Mlandizi? Ninakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEQUIP), Serikali imeendelea kutoa fedha, kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za kata. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tuna orodha ya kata zote zenye vigezo ambazo hazijapata shule za sekondari na kazi inayoendelea sasa ni kupata fedha, kwa ajili ya kwenda kujenga shule hizo. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mwakamo kwamba, kata zake hizo mbili zitapelekewa fedha, kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari. Ahsante.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa hii nafasi. Kata ya Akheri imetenga eneo katika Kitongoji cha Maksoru, Kijiji cha Nguruma, kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya na wananchi wameshaanza kujitolea, kwa ajili ya ujenzi huo. Je, Serikali ina mkakati gani wa kutenga fedha, kwa ajili ya kujenga hiyo sekondari? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Dkt. Pallangyo alikwishawasilisha hoja hiyo Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Natumia nafasi hii kuwapongeza wananchi wa Kata hiyo ya Akheri pamoja na kijiji hicho kwa kutenga eneo na kuanza kutumia nguvu zao katika ujenzi wa sekondari.
Mheshimiwa Spika, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge na Wananchi wa Jimbo la Arumeru kwamba, Serikali hii sikivu itapeleka fedha, ili kuhakikisha shule hiyo inakamilika na wananchi na watoto wetu wanapata maeneo jirani na bora zaidi, kwa ajili ya kupata elimu.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?
Supplementary Question 4
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, miundombinu ya Shule Kongwe ya Kata ya Mogabiri ambayo imepandishwa hadhi na kuwa ya Kidato cha Tano na Sita ni chakavu sana. Nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba, inakarabati miundombinu ile, ili iweze kuendana na majengo ya kisasa ambayo mnajenga na kuweka mazingira safi kwa wanafunzi kujifunza? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ulianza na ukarabati wa shule za sekondari za kitaifa ambazo zote zimekarabatiwa, lakini tunaendelea na ukarabati wa shule zote chakavu ili kuwezesha mazingira ya wanafunzi wetu kusoma katika mazingira bora zaidi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Esther Matiko kwamba, shule hiyo ya sekondari itapewa kipaumbele, ili fedha iweze kupatikana, kwa ajili ya ukarabati na kuboresha miundombinu chakavu ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira bora zaidi. Ahsante sana.
Name
Charles Muguta Kajege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?
Supplementary Question 5
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, wananchi wa Kisiwa cha Nafubo wameanza kuchangia, kwa ajili ya ujenzi wa sekondari yao. Je, ni lini Serikali itawashika mkono ili kukamilisha zoezi hilo? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, moja ya vipaumbele vya juu kabisa ni kujenga miundombinu ya huduma za jamii, ikiwemo shule katika maeneo magumu kufikika kijiografia na hususan maeneo ya visiwa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwanza tunawapongeza wananchi hao kwa kuanza na tunawatia moyo waendelee kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa shule hiyo ya sekondari. Serikali hii sikivu itawashika mkono kwa kupeleka fedha ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ya sekondari.
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini?
Supplementary Question 6
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, Kata ya Mwasubi ni moja kati ya kata ambazo hazina shule za sekondari na wanafunzi wamekuwa wakisafiri kwenda Sekondari ya Bunambiu. Nguvu za wananchi zimeshaanza kuchangiwa na sasa ujenzi wa madarasa mawili upo katika hatua ya lenta, unakwenda vizuri. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba, inaweka nguvu za kutosha kukamilisha ujenzi huo?
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA – (MHE. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, namhakikishia tu Mheshimiwa Butondo kwamba, Mpango wa Serikali ni kujenga shule za sekondari za kata kila kata. Nawapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kuanza kwa nguvu zao na waendelee kufanya hivyo, wakati Serikali inatafuta fedha, kwa ajili ya kwenda kukamilisha shule hiyo ya sekondari. Ahsante sana.