Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 134 2025-02-06

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini kuzalisha asali kwa kuwa kuna idadi kubwa ya miti inayoweza kutundikwa mizinga?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa ufugaji nyuki kwenye kuimarisha uhifadhi na kuongeza kipato cha wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini Serikali kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania imewezesha miradi minne ya ufugaji nyuki yenye thamani ya shilingi 32,270,000 kwa Shule ya Sekondari Komakya, Kikundi cha Jikomboe cha Kijiji cha Komela, Mradi wa Uanzishwaji wa Kitalu cha Miti na Upandaji Miti katika Shule ya Sekondari ya Weruweru na Mradi wa Uanzishwaji wa Vitalu vya Miti na Kuhamasisha Upandaji Miti katika Kata ya Mwika Kusini.

Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania inaendelea kuwajengea uwezo wafugaji nyuki wa Wilaya ya Moshi Vijijini, ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 imepanga kuwezesha mizinga 40 na vifaa vingine vya ufugaji nyuki. Katika kuongeza wigo wa wanufaika wa miradi ya ufugaji nyuki, Wizara kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi katika Wilaya ya Moshi Vijijini kuhusu namna ya kuandaa na kuwasilisha maandiko ya kuomba ruzuku kwenye mfuko wa misitu.