Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini kuzalisha asali kwa kuwa kuna idadi kubwa ya miti inayoweza kutundikwa mizinga?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali y a nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Wafugaji wengi wa nyuki katika Halmashauri ya Moshi na maeneo mengine ya vijijini Tanzania wanakosa elimu ya mbinu bora ya ufugaji wa nyuki. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha program za mafunzo haya kwa wananchi wetu hawa kupitia kwa Maafisa Ugani wa Nyuki hapa nchini?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Moja ya changamoto kubwa inayowakabili wafugaji nyuki wetu hapa nchini na hasa wale wa Jimbo la Moshi Vijijini na maeneo mengine ni ukosefu wa vifaa bora vya kufugia nyiki kama mizinga ya kisasa. Je, Serikali ina mikakati gani au mipango gani ya kutoa ruzuku kwa wafugaji hawa wa nyuki ili wapate hizi dhana waweze kufuga nyuki kwa uhakika?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa kuelewa kwamba sekta hii ili ikue suala la elimu ni muhimu. Serikali inaendelea kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki katika chuo chetu cha ufugaji nyuki Tabora, lakini vile vile inatoa mafunzo kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mheshimiwa Spika, wataalam hawa wanaopata mafunzo kwenye eneo hili wanatumika kwa kuajiriwa kwenye halmashauri zetu lakini vile vile wanaajiriwa na taasisi yetu ya TFS. Kupitia taasisi hizi na halmashauri zetu Serikali iliandaa mpango maalum wa mafunzo ambao unatumika na wataalam hawa kutoa mafunzo kwa wananchi kwenye maeneo yetu.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili kuhusu ruzuku ya vifaa. Serikali kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania ina mpango wa kutoa ruzuku kwa halmashauri zetu, lakini vile vile kwa wananchi wanaojiingiza kwenye Sekta hii ya Ufugaji wa Nyuki.
Mheshimiwa Spika, napenda kuwafahamisha wananchi kwa ujumla kwamba tayari dirisha la kuomba ruzuku kupitia Mfuko wa Misitu limekwishafunguliwa. Dirisha hili litakuwa wazi mpaka mwezi Machi. Hivi nitoe rai kwa halmashauri zetu na wananchi wote kuitumia fursa hii ili kuweza kupata ruzuku ya ufugaji nyuki pamoja na vifaa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved