Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 148 2025-02-07

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:-

Je, ni Mkakati upi Serikali imeuweka kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao ili kuwasaidia wakulima wasipate hasara?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ili kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao nchini, Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na Mamlaka ya Udhibiti Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeweka mikakati ifuatayo:-

(i) Kutambua na kusajili waagizaji wote wa pembejeo nchini ili kudhibiti uingizaji holela wa pembejeo nchini;

(ii) Kufanya ukaguzi wa kila shehena ya pembejeo za kilimo inapofika bandarini au mpakani na kuchukua sampuli kwa ajili ya uchambuzi wa kimaabara;

(iii) Kutoa elimu kwa wakulima na wauzaji wa pembejeo za kilimo kuhusu utambuzi wa pembejeo feki, utunzaji na matumizi bora ya pembejeo; na

(iv) Kufanya kaguzi za mara kwa mara katika maghala na maduka ya pembejeo na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika ikiwemo kuwafutia leseni za kuuza pembejeo zote wale wote wanaobainika kuuza au kusambaza pembejeo feki.

SPIKA: Mheshimiwa Cecilia Paresso, swali la nyongeza. Mheshimiwa Mwandabila alikuwa hajasimama, kwa hiyo, nikafiri hana swali la nyongeza. Kumbe unayo? Haya, Mheshimiwa Cecilia Paresso halafu nitakurejea.