Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, ni Mkakati upi Serikali imeuweka kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao ili kuwasaidia wakulima wasipate hasara?
Supplementary Question 1
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Pamoja na utaratibu uliopo wa Serikali wa kutoa hizo mbegu za ruzuku lakini mawakala wanakuwa wachache sana. Kwa mfano, Jimbo la Karatu mawakala ni watatu tu kwa wilaya nzima, je, Serikali ina mpango gani wa kupanua wigo ili wananchi wengi wafaidike na hizo mbegu za ruzuku? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwamba mawakala tumetoa fursa kwa wafanyabiashara wote wanaotaka kuingia katika biashara ya mbegu pamoja na mbolea kuja kujisajili. Wanajisajili TFRA halafu wanapewa hicho kibali cha kuuza mbolea. Kwa hiyo, ni room ya kila mtu ambaye anahitajika kufanya hivyo. Kwa hiyo, niseme tu kabisa kwamba wale wote wanaohitaji kufanya hiyo biashara waje na sisi tutawapa hiyo ruhusa ya kufanya biashara hiyo, ahsante sana.
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, ni Mkakati upi Serikali imeuweka kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao ili kuwasaidia wakulima wasipate hasara?
Supplementary Question 2
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, samahani nilikuwa nimepitiwa kidogo.
Mheshimiwa Spika, nilitaka kufahamu, kwa kuwa Serikali imeweka njia mbalimbali ambazo ni thabiti za udhibiti wa uingizaji wa pembejeo, lakini wakulima wanakutana na pembejeo feki. Je, Serikali haioni kuwa kuna mahali imefeli katika udhibiti huo wa uingizaji wa pembejeo feki?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Je, ni fidia zipi hutolewa kwa wakulima ambao huathirika na matumizi ya pembejeo feki? Ahsante. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nikubaliane na Mheshimiwa Neema kwamba, kweli kuna changamoto kwenye baadhi ya maeneo hususan maeneo ya mipakani hasa kwa zile mbolea ambazo zinapitishwa kutoka nchi jirani kuingia ndani.
Mheshimiwa Spika, jukumu letu sisi kama Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, tumeendelea kuongeza udhibiti wa kuongeza Watendaji ambao wamekuwa wakifanya patrol za mara kwa mara. Kwa hiyo, kikubwa tu ni sisi kuendelea kuongeza huo udhibiti ili kuhakikisha kwamba tunafanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la fidia kwa wakulima ambayo inatokana na mbolea feki, moja, kwa hatua ya sasa ambayo tumekuwa tukiifanya, wale wote ambao wanatambulika ama kubainika wamepeleka mbolea feki, tunawachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwapeleka Mahakamani, kuwafutia leseni na kuendelea. Baada ya hapo maana yake Mahakama ndiyo itakayoamua maamuzi ya mwisho juu ya hatua gani za kisheria pamoja na za kifidia ambazo mwananchi anapaswa kulipwa. Kwa hiyo, hiyo ndiyo hatua tuliyopo kwa sasa, ahsante.
Name
Jenista Joackim Mhagama
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Peramiho
Primary Question
MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:- Je, ni Mkakati upi Serikali imeuweka kudhibiti uingizaji wa pembejeo feki za mazao ili kuwasaidia wakulima wasipate hasara?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Madaba ni miongoni mwa wananchi walioathirika sana na mbegu feki ambazo zilisambazwa msimu uliopita. Wapo wengi wamepata hasara kabisa katika mashamba yao, na kwa vile yule ambaye alisambaza hizo mbegu feki alishakamatwa.
Mheshimiwa Spika, je, Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha kwamba hasa wakulima waliopata hasara kwa kutumia zile mbegu wanafidiwa? Ahsante. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nilikuwa najibu katika swali ambalo lilitangulia, ni kwamba, baada ya yule msambazaji wa mbegu feki au pembejeo feki kukamatwa, sisi kama Wizara hatua ambazo tumechukua ni kumfutia leseni ya kushiriki katika shughuli zote za mazao ya kilimo.
Mheshimiwa Spika, hatua ya pili, tumeshapeleka Mahakamani, na jambo hili lipo katika hatua za kisheria. Kwa hiyo, baada ya hatua za kisheria, ninaamini sasa tunaweza tukawa na neno la kusema kuliko kuingilia Mahakama, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved