Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 156 2025-02-07

Name

Seif Khamis Said Gulamali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manonga

Primary Question

MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: -

Je, ni lini Kata za Ntobo, Ngulu, Igoweko, Ugaka na Sungwizi ambazo zinaongoza kwa mifugo nchini zitapatiwa fedha za ujenzi wa majosho?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/2025, Wizara haikuweka katika mpango wa bajeti ujenzi wa majosho maeneo mbalimbali hapa nchini, ili kutoa fursa ya uwepo wa kampeni kubwa ya chanjo ya Kitaifa ambayo itahusisha uchanjaji wa magonjwa ya homa ya mapafu ya ng’ombe (CBPP), sotoka ya mbuzi na kondoo (PPR) na ugonjwa wa kideri au mdondo kwa kuku. Kampeni hii inatarajiwa kuanza mwezi Februari, 2025 kwa kuwa, taratibu zote zimekamilika.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuweka katika Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2025/2026 ujenzi wa majosho nchini, yakiwemo majosho ya Kata za Ntobo, Ngulu, Igoweko, Ugaka na Sungwizi. Hata hivyo, Wizara inaielekeza Halmashauri ya Igunga kutenga fedha zinazopatikana katika mapato yake ya ndani ili kujenga majosho kwa ajili ya kuwasaidia wananchi katika maeneo husika.