Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 22 2025-01-29

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapandisha hadhi Shule ya Sekondari ya Rubanga iliyopo Geita kuwa ya kidato cha tano na sita?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, shule za kidato cha tano na sita za bweni ni za Kitaifa na huchukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini. Jimbo la Geita kwa sasa lina shule moja ya kidato cha tano na sita ambayo ni Bugando.

Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari ya Rubanga bado haijakidhi vigezo vya kuipandisha hadhi kuwa ya kidato cha tano na sita ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mabweni, bwalo na madarasa ya kutosha. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili Shule ya Rubanga iwekwe kwenye mpango wa kupandishwa hadhi kuwa ya kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya shule za sekondari ikiwemo Shule ya Sekondari ya Rubanga kadiri ya upatikanaji wa fedha.