Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:- Je, lini Serikali itapandisha hadhi Shule ya Sekondari ya Rubanga iliyopo Geita kuwa ya kidato cha tano na sita?

Supplementary Question 1

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu ya Serikali. Katika halmashauri hii, je, ni lini Serikali itapandisha hadhi Shule ya Sekondari Evarist iliyopo Nyarugusu kutoka Wilaya ya Geita kuwa kidato cha tano na cha sita?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba kumpa majibu Mheshimiwa Tumaini Magessa kuhusiana na swali lake hilo kwamba Serikali itaendelea kufanya tathmini na kupita kufanya verification katika shule mbalimbali Tanzania nzima ikiwemo katika jimbo lake. Shule hii ya Evarist na yenyewe itapitiwa ili kufanya uhakiki na kufanya tathmini na kuleta fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ambayo inahitajika kwa ajili ya shule kuwa na vigezo vya kupandishwa kuwa kidato cha tano na cha sita. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kazi hiyo itafanywa na Serikali ili shule hizi zipandishwe hadhi na ziweze kuwanufaisha wanafunzi wetu.