Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Good Governance Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 23 2025-01-29

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:-

Je, kwa nini watumishi wa afya wasijaze ripoti za utendaji kazi kila mwezi badala ya kila wiki ili wapate muda zaidi kuhudumia wagonjwa?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, lengo la utoaji taarifa za utekelezaji wa mipango ya Utendaji Kazi ya Watumishi wa Umma katika vipindi tofauti ni kuwezesha kubaini mwelekeo wa utekelezaji katika kufikia malengo ya taasisi kwa ujumla. Aidha, taarifa za utekelezaji wa mipango ya utendaji kazi ya watumishi zinajadiliwa katika vikao vya taasisi vinavyofanyika kila wiki kwa lengo la kubaini hali ya utendaji kazi wa taasisi husika kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, watumishi wa afya na watumishi wengine wa umma wanapaswa kuendelea kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango yao ya utendaji kazi katika kipindi cha siku, wiki na kadri itakavyohitajika. Lengo ni kubaini changamoto zinazojitokeza kipindi cha utekelezaji na kuweka mikakati ya kuzitatua kwa wakati. Ninashukuru.