Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Je, kwa nini watumishi wa afya wasijaze ripoti za utendaji kazi kila mwezi badala ya kila wiki ili wapate muda zaidi kuhudumia wagonjwa?
Supplementary Question 1
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kukagua au kutoa ripoti ni suala muhimu sana katika kuwasimamia wafanyakazi, lakini kada ya afya ni kada muhimu sana ambayo inaokoa maisha ya watu. Hamwoni kuna namna kwa kada hii pekee ikapewa nafasi ya kutoa kwa mwezi badala ya kila siku, kwa sababu saa 24 ni saa za kuangalia wagonjwa? Ahsante.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwakagenda, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, utaratibu wa upimaji watumishi kupitia PEPMIS tumeweka kwa muda kwa wiki kwa makusudi maalum kwamba tuweze kutambua tatizo kwa muda mfupi na kulitatua. Kuweka muda wa mwezi mmoja haitaweza kutusaidia kwa sababu tutakosa kupata consistency ya majukumu aliyoyafanya mtumishi kwa sababu itakuwa ni muda mrefu. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge na tangu tumeanza zoezi hili hatujapata malalamiko ya hawa watumishi moja kwa moja, kwamba jambo hili linawasumbua, wameendelea kujaza hiyo PEPMIS kwa wakati na mpaka sasa zoezi hili linaendelea vizuri. Ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved