Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 26 2025-01-29

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza bei ya gesi ya matumizi ya nyumbani kwani wananchi wengi wamepata mwamko?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024 – 2034 ambapo pamoja na masuala mengine, Serikali imejikita katika kuhakikisha inapunguza bei ya gesi ya mitungi ya kupikia (LPG). Vilevile, Serikali inaendelea na utoaji wa ruzuku ya 20% – 50% ya bei ya mitungu ya gesi ya LPG kwa watumiaji wa mwisho. Aidha, Serikali itaendelea kuja na mikakati mingine ili kuhakikisha bei ya gesi inapungua. Ahsante.