Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza bei ya gesi ya matumizi ya nyumbani kwani wananchi wengi wamepata mwamko?

Supplementary Question 1

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza mawakala wa gesi vijijini ili kuwasaidia wananchi kupata huduma kwa urahisi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza vituo vya kujazia gesi kwenye magari maeneo yote nchini ikiwemo Zanzibar? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, moja, kwenye upande wa kuongeza mawakala, tayari tumeanza mazungumzo na kampuni za LPG ili kuhakikisha tuna-map maeneo yote ili wananchi wakitaka kujaza gesi, basi wajaze gesi hiyo kwenye mitungi kwa urahisi. Tunaendelea na mikakati hii, mpaka sasa tumefikia tu miezi sita ya utekelezaji wa mkakati. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunalifanyia kazi kwa ufanisi mkubwa sana ili wananchi waweze kujaza gesi kwa urahisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na vituo vya kujaza gesi kwenye magari, kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vituo mbalimbali, kwa Dar es Salaam tuna ujenzi wa vituo vitatu ambavyo tunajenga kwa ajili ya kupunguza foleni ambayo ipo katika vituo vya CNG. Vilevile, kwa kushirikiana na sekta binafsi tunavyo vituo vingine ambavyo tunavijenga lakini kupitia Shirika letu la Maendeleo ya Petroli, tunanunua vilevile magari ya kuhamishika kwa ajili ya kuhakikisha barabara nzima kuanzia Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma kuna vituo hivi kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi wanaotaka kujaza gesi kwenye magari.

Mheshimiwa Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tunaendelea kulifanyia kazi jambo hili kwa ufanisi mkubwa sana ili wananchi waendelee kuwa na moyo wa kuweka mifumo ya gesi kwenye magari yao.

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza bei ya gesi ya matumizi ya nyumbani kwani wananchi wengi wamepata mwamko?

Supplementary Question 2

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa pamoja na kupunguza bei ya gesi, kuna maeneo ambayo bado haitakuwa nafuu zikiwemo nyumba za malezi za masista kama Huruma. Serikali ina mpango gani wa kuwapa ruzuku maeneo hayo ili waweze kuwa na ile mitungi mikubwa ya mapipa?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwa kweli maeneo hayo ni maeneo muhimu sana kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge. Kwa sababu tunaendelea na utekelezaji wa mkakati huu tunaomba watupe muda, tutakuja na mikakati ambayo kwa kweli itakuwa jumuishi kwa aina zote za makundi katika jamii. Ahsante. (Makofi)