Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Health and Social Welfare Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 119 2025-02-05

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMINA HAJI ABASS aliuliza:-

Je, Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo wa Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) imeleta matokeo gani tangu kuzinduliwa?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu kuanzishwa kwa Kampeni Huru ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania yaani SMAUJATA, Tarehe 16 Juni, 2022, kampeni imeweza kuhamasisha wananchi 10,714 kutoka Tanzania Bara na 191 kutoka Zanzibar kujiunga na Kampeni hiyo kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba, 2024.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kampeni imeongeza hamasa ya jamii ya kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kupitia wana SMAUJATA na watendaji wengine, hivyo kusababisha jumla ya matukio 2,533 ya ukatili wa kijinsia na watoto katika mikoa yote kubainika na kuwasilishwa katika mamlaka za usimamizi wa sheria, kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kampeni ya SMAUJATA imeongeza uelewa wa jamii kuhusu vitendo vya ukatili kwa kuwa, uongozi wa kampeni ya SMAUJATA upo kuanzia ngazi ya huduma za msingi mpaka Taifa. Aidha, kampeni hii imepunguza pengo la upungufu wa wataalam wanaotakiwa kutoa elimu ya ukatili katika jamii, hasa ikizingatiwa kuwa, kuna upungufu wa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii ikilinganishwa na mahitaji halisi.