Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMINA HAJI ABASS aliuliza:- Je, Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo wa Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) imeleta matokeo gani tangu kuzinduliwa?

Supplementary Question 1

MHE. TAMINA HAJI ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili. Swali la kwanza; je, kampeni hii ni ya muda mrefu au ni endelevu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Serikali za Mikoa na Wilaya zinashiriki vipi katika kampeni hii? Ahsante.

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Tamina, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa kampeni hii ina muda wa miaka mitatu. Vilevile, kampeni hii ya SMAUJATA imeungwa na Wizara ya Mambo ya Ndani na wamejisajili kama NGO. Pia, inafanya kazi katika taasisi zote za Serikali kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Serikali, Mikoa pamoja na Wilaya zinashirikiana vema kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ukatili na utekelezaji mbalimbali wa kupinga ukatili. Ahsante.