Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 120 2025-02-05

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-

Je, kwa nini Serikali isiboreshe barabara zote nchini kwa kuongeza barabara za waenda kwa miguu na pikipiki?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inahakikisha kuwa barabara zote mpya zinazojengwa kwa kiwango cha lami zinahusisha ujenzi wa njia za waenda kwa miguu katika maeneo ya majiji, miji na maeneo yaliyojengeka. Kwa barabara ambazo zilijengwa bila kuweka njia za waenda kwa miguu maboresho yamekuwa yanafanyika kwa kujenga njia za waenda kwa miguu kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.