Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, kwa nini Serikali isiboreshe barabara zote nchini kwa kuongeza barabara za waenda kwa miguu na pikipiki?

Supplementary Question 1

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Majibu ya Serikali kwa kweli yanasikitisha sana. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; tumeendelea kupoteza Watanzania waenda kwa miguu na waendesha pikipiki hata jana tu tulishuhudia ajali mbaya sana hapo Meriwa na raia wawili wakafariki. Nataka kujua Serikali imejipanga vipi, mathalani unapokuwa unaenda Dar es Salaam waendesha pikipiki wale wanaobeba mkaa, wanabeba mkaa mwingi inaziba hata visibility ambapo inapelekea ajali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajipanga vipi wakati wanaendelea na mkakati wa kujenga barabara hizo walizosema kuhakikisha kwamba Sheria ya Usalama Barabarani inatekelezeka na hawa watu wanaoendesha pikipiki wanafuata hizo sheria ili wasipoteze maisha ya Watanzania?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kumekuwepo na mwingiliano mkubwa hasa kwenye hizi highway zetu, ukiacha pikipiki utakutana na kondoo, utakutana na mbuzi, utakutana na mbwa, utakutana na wanyama wengine mbalimbali. Wizara hii inashirikiana vipi na Wizara nyingine kama za Mifugo ili waweze kuhakikisha kwamba hawa raia wenye mifugo hii wanahakikisha haingii barabarani na kusababisha ajali za hapa na pale?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza katika jibu langu la msingi kwamba tunakiri kwamba barabara zilizojengwa zamani hazikuwa na hizo facilities, lakini barabara zote tunazozijenga sasa hivi kwenye miji, miji mikubwa hata miji inayokua sasa hivi tunazingatia kwamba hicho kinafanyika, tunayo mifano ya hizo barabara nyingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, kwa mfano Dodoma hapa ukienda kwenye barabara ya outer ringroad utakuta hizo facilities zote zipo lakini tuna mpango pia barabara zote zinazotoka katikati ya mji kwenda kuunga na hiyo ringroad tutahakikisha kwamba ziko kwenye design na zitajengwa. Tunayo barabara tunasema inner ring lakini kuna median kwa Dodoma hapa barabara zote hizo tutazingatia hicho unachokisema. Hilo la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wale wanaotumia tuna sheria pia ambazo zinamtaka kila anayetumia barabara hizi afuate sheria ambazo zipo zinatumika. Suala la waendesha pikipiki ambao wanavunja sheria vipo vyombo vingine ambavyo vinashughulika nao, ndiyo maana wanachukuliwa hatua kwa sababu sheria hizo zipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imejipanga na barabara ambazo tunajenga ukienda BRT, ukienda madaraja ya Tanzanite, Kigongo – Busisi, tunazo barabara tume-design Mwanza ambazo tutazijenga njia nne zote zimezingatia hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu cha msingi ni kwamba wote tunaotumia barabara, anayetumia chombo cha moto, lakini wale pia wanaotembea tume-design na tuna sheria inayosema mifugo ni marufuku kupita kwenye barabara. Kwa hiyo, anayepitisha mifugo ama amebeba mkaa kinyume cha taratibu huyo anavunja sheria na sheria zipo ndiyo maana watu hao wanachukuliwa hatua. Kwa hiyo, tunashirikiana vizuri sana na vyombo vya usalama wenzetu wa Polisi ambao wapo na ndiyo maana zile sheria ndiyo zinazowafanya hawa watu wachukuliwe hatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo nichukue nafasi hii kuwajulisha...

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, kwa nini Serikali isiboreshe barabara zote nchini kwa kuongeza barabara za waenda kwa miguu na pikipiki?

Supplementary Question 2

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi Novemba ulikuwa umekaa kwenye hicho kiti, nikauliza swali la Barabara ya Tarime - Nyamongo ninavyozungumza barabara ile mkandarasi hayupo, njia ya pembezoni imeharibika, waenda kwa miguu hawapiti na magari hayapiti ni matusi kule Tarime. Je, ni nini kauli ya Serikali kwa jambo hili? Nashukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nimjulishe Mheshimiwa Mbunge kwamba alichouliza swali la msingi hapa ni barabara ambazo zimetumika na kuwatengenezea waenda kwa miguu ama baiskeli njia tofauti.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninalosema hii ni barabara za mchepuko za muda kwa maana ya diversion ambazo mkandarasi aliyepo anayejenga barabara hiyo ya Tarime kwenda Nyamongo anatakiwa ajenge diversion na ni wajibu wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kama barabara hizo hazipitiki na kwa kuwa ni barabara ambazo zipo kwa ujenzi kwa sasa na zinatumika kwa muda nimweleze tu Meneja wa Mkoa wa Mara ahakikishe kwamba huyo mkandarasi anatengeneza hizo barabara na wananchi wanapita bila kukwama. Ahsante.