Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 122 2025-02-05

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza:-

Je, baada ya Serikali kulipa eneo la Liganga na Mchuchuma lini uwekezaji unaanza?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha kulipa fidia ya eneo la Liganga na Mchuchuma ikiwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Company limited ambaye ndiye alikuwa Mwekezaji wa mradi huo, ilitoa taarifa ya kwamba ipo katika hatua za mwisho za kuuza hisa zake katika Kampuni ya Shudao Group ya China.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kampuni hii ya Shudao Group ndiyo itakayotekeleza mradi huu muhimu baada ya taratibu za kuhamisha hisa kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia Februari, 2025. Kwa hiyo, ni matarajio ya Serikali kuwa mradi huu utaanza kutekelezwa ndani ya mwaka wa fedha 2025/2026. Nakushukuru.