Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza:- Je, baada ya Serikali kulipa eneo la Liganga na Mchuchuma lini uwekezaji unaanza?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na niipongeze sana Serikali kwa kutatua mgogoro wa kimkataba kwa njia za kidiplomasia na leo tunasonga mbele. pamoja na pongezi hizi nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; pale eneo la Liganga kuna mradi mdogo wa Maganga Matitu, kuna wananchi wachache walikuwa bado hawajalipwa fidia waliahidiwa hadi Januari hii watakuwa wamelipwa fidia. Je, ni lini fidia hizo zitalipwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali dogo la pili; kule Nkomang’ombe kuna eneo dogo la makaa ya mawe Ketewaka nako kuna wananchi wachache walikuwa hawajalipwa fidia zao. Je, ni lini sasa Serikali hii iliyoweza kulipa bilioni 15 itawamalizia wananchi hawa ili waweze kufanya shughuli zao kwenye maeneo mengine? (Makofi)

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge Kamonga kwa ufuatiliaji wa mradi huu na ni nimpe pongezi kwa sababu ameweka historia kati ya Wabunge ambao mradi huu sasa unatekelezwa ambao ulikuwa mradi wa kihistoria chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye anaweka naye historia kwa mradi huu muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna miradi hii mingine miwili ambayo inatekelezwa katika Jimbo la Ludewa ikiwemo huu wa Maganga Matitu ambao uko chini ya mwekezaji Fujian Industry Tanzania Limited ambaye kimsingi ndiye anatakiwa kulipa fidia na tayari tumeshakubaliana naye mpaka kufikia mwezi Machi awe amelipa fidia ambayo inafikia takribani bilioni 4.2. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Ludewa katika eneo hili kwamba nao watalipwa fidia yao kama ambavyo tulipanga.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali kadhalika kwenye eneo hili la Nkomang’ombe ambako kuna Mradi huo wa Ketewaka chini ya Mwekezaji M.M. Steel ambaye naye pia kama mwekezaji kutokana na makubaliano ya Serikali ndiye anayetakiwa kulipa fidia. Tuko kwenye majadiliano naamini ndani ya mwaka huu wa fedha kwa maana ya mwaka 2024/2025 kufikia mwezi Juni atakuwa amelipa fidia ambayo inafikia takribani 2.1. Nakushukuru sana. (Makofi)

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza:- Je, baada ya Serikali kulipa eneo la Liganga na Mchuchuma lini uwekezaji unaanza?

Supplementary Question 2

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Awali ya yote na mimi naipongeza sana Serikali kwa hatua hii kubwa ambayo tumeisikia kwa mara ya kwanza ndani ya Bunge lako kwamba sasa mwekezaji atakayetekeleza mradi amepatikana na ndani ya miezi mitatu tutakuwa na huo uwekezaji.

Je, Serikali haioni haja ya kuwahusisha Watanzania kwenye uwekezaji huu mkubwa wa Liganga na Mchuchuma ili tutengeneze mabilionea? (Makofi)

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Deo Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, lakini ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kwa sababu ndiye amekuwa pia anasimamia kuhakikisha mradi huu unakamilika na leo tunaona matunda haya chini ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli moja ya mikakati ya Serikali ni kuona namna gani Watanzania wazawa nao wanafaidika na mradi huu mkubwa wa kihistoria ambao ni wa Mchuchuma na Liganga.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mkataba ule Serikali ina hisa kupitia Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC) takribani 20% ambazo hizo ndiyo zitatumika kuwapa wazawa nafasi ya kushiriki aidha kwa kuuza hisa katika Stock Exchange au pia na wao kuingia katika kutekeleza mradi huu. Kwa hiyo, watashiriki katika kutekeleza mradi huu muhimu kupitia hizo 20% ambazo zitaongezeka kadri tunavyokwenda kwa maana tumekubaliana ifike mpaka 49%. Kwa hiyo, Serikali ikinunua hizo hisa maana yake ni nafasi ya Watanzania kushiriki katika kutekeleza mradi huu muhimu wa kimkakati. Nakushukuru sana. (Makofi)