Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 7 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 123 | 2025-02-05 |
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. CHARLES J. MWIJAGE aliuliza:-
Je, nini mpango wa Serikali kutekeleza miradi ya maji katika Kata tano za Ziwani, Kata za Muleba Magharibi na Gwanseli – Kagoma?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la Ziwa Wilayani Muleba lina jumla ya Kata tano za Goziba, Bumbire, Mazinga, Ikuza na Kerebe ambazo pamoja na kuwa ziwani zina tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ni kufanya usanifu wa kina wa miradi, detailed design na kutatua tatizo hilo. Aidha, Skimu ya Iroba, Kinagi, Goziba na Ikuza zinafanyiwa ukarabati katika mwaka huu wa fedha 2024/2025.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa eneo la Muleba Magharibi lenye Kata za Kasharunga, Karambi, Kyebitembe, Mubunda, Burungura, Nyakatanga, Mushabago, Ngenge pamoja na Rutoro kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali itafanya upembuzi yakinifu wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria ili kuhudumia Kata hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kupitia program za uchimbaji wa visima 900 Serikali tayari imechimba visima 14 na ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma (point source) unaendelea. Utekelezaji wa kazi hizo unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2025 na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Gwanseli na Kagoma zinapata huduma ya maji kupitia Skimu ya Ilemela na Kagoma. Aidha, katika kuhakikisha Jimbo la Muleba Kaskazini linapata huduma ya maji ya uhakika, Serikali imekamilisha usanifu wa Mradi wa Kutoa Maji Ziwa Victoria kwa ajili ya kuhudumia Kata sita za Gwanseli, Magata, Karutanga, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma ambapo unatarajiwa kutekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved