Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. CHARLES J. MWIJAGE aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali kutekeleza miradi ya maji katika Kata tano za Ziwani, Kata za Muleba Magharibi na Gwanseli – Kagoma?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; katika eneo ambalo Serikali inaendelea kuchimba, wameshachimba 14 na kazi inaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, wameanza kujenga vituo vya kutolea maji point of service, lakini kuna wadau Christian Church of Tanzania na Fimbo ya Musa (The Orthodox) wamechimba visima 16. Je, kwa nini sasa Serikali kwa usanifu mzuri na ujenzi ambao yenyewe inajenga visima vyake, isiwasaidie wadau hawa kusudi hii kazi nzuri ya Serikali ikaenea kwenye visima vyote?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika Mradi wa Kagoma Serikali imejenga tanki zuri nashukuru kwa hilo, lakini usambazaji wa maji haujafika katika Vijiji vya Nsisha, Kikuku na Bigaga. Ni lini Serikali sasa itapeleka neema hii nzuri kwenye vijiji hivyo kusudi watu wafaidi kazi ya Awamu ya Sita? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nampongeza sana Mheshimiwa Charles Mwijage kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali ndani ya jimbo lake na kutambua Wizara ya Maji kuchimba visima 14 na point sources zinaendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali. Ni jukumu la Serikali na Sera yetu ya Maji kuhakikisha kwamba tunashirikiana na wadau wote wanaotoa huduma ya maji katika maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba katika eneo ambalo wadau, iwe taasisi ya kidini, wananchi wenyewe wameweza kutoa huduma au wameweza kuchimba visima, lakini wameshindwa kuviendeleza, Serikali iko tayari kuendelea kushirikiana nao ili kuboresha visima hivyo ili viweze kutoa huduma ambayo inakusudiwa na wananchi, lakini maji yawe safi na salama kwa mujibu wa taratibu za Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la nyongeza ni kuhusu Mradi wa Kagoma. Ni kweli Serikali tayari imewekeza fedha za kutosha katika ujenzi wa tenki lile. Katika bajeti ya mwaka uliopita tuliweza kujenga tenki lile, lakini hatukuwa na bajeti ya kujenga mtandao wa maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ni Mjumbe katika Kamati yetu ya Maji na Mazingira, nimwombe, kupitia Bunge lako Tukufu, tutakapofikisha kwenye Kamati aweze kuwa sehemu ya kuhakikisha kwamba tunapitisha bajeti ambayo itatuwezesha kuongeza mtandao wa maji katika maeneo ya Vijiji vya Kikuku na maeneo mengine ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja ili wapate huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana.
Name
Hassan Seleman Mtenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. CHARLES J. MWIJAGE aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali kutekeleza miradi ya maji katika Kata tano za Ziwani, Kata za Muleba Magharibi na Gwanseli – Kagoma?
Supplementary Question 2
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Jimbo la Mtwara Mjini bado linakabiliwa na upungufu wa maji. Je, ni lini Serikali itaamua kuyaleta maji kutoka Mto Ruvuma hadi katika Jimbo la Mtwara Mjini ili tuweze kupata maji kwa wingi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Mtenga kwa kazi kubwa anayoifanya pale Mtwara. Hakika amekuwa akitupatia ushirikiano mzuri sana na Serikali imeshaamua kuhakikisha kwamba tunakuwa na Gridi ya Taifa ya Maji kutoka kila angle ambapo tuna uwezo wa kupata chanzo cha maji cha uhakika na kwa sababu Mto Ruvuma ni chanzo cha uhakika, nimhakikishie Mbunge kwamba Serikali tayari imekwishaamua na tumeshafanya usanifu.
Mheshimiwa Naibu Spika, bado tunatafuta fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunatekeleza mradi huo. Pesa zitakapopatikana Mheshimiwa Mbunge, mradi huo utaanza kutekelezwa kwa ajili ya wananchi wa Mtwara. Ahsante sana.
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHARLES J. MWIJAGE aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali kutekeleza miradi ya maji katika Kata tano za Ziwani, Kata za Muleba Magharibi na Gwanseli – Kagoma?
Supplementary Question 3
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kuniona. Jimbo la Bukoba Vijijini, Kata ya Lukoma, Kijiji cha Nsheshe, maji ni ya shida sana, napenda kujua ni lini Serikali itaenda kuwatua ndoo akinamama wa kijiji hiki?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Oliver kwa kuendelea kuwapambania wananchi wa Kagera na kushirikiana na Wabunge wenzake wa majimbo. Vilevile, natambua changamoto ya eneo la Nsheshe ambalo amelitaja. Kwa kumbukumbu zangu kuna Mradi mmoja wa World Vision katika eneo lile unao-serve huduma ya maji pale katika eneo linaloitwa Karama.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, tumechimba visima ambavyo tunatarajia tukipata fedha tutafanya usanifu wa kwenda sasa kutengeneza mtandao wa maji ambao utaenda kuwafikia wananchi wote wa eneo husika. Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo lake kuu ni kumtua mama ndoo kichwani na kupata maji safi na salama, toshelevu na yenye gharama nafuu. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved