Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 7 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo | 124 | 2025-02-05 |
Name
Rashid Abdallah Shangazi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlalo
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:-
Je, fursa zipi zitapatikana kwa Mtanzania mmoja mmoja na vikundi kupitia Fainali za Mpira wa Miguu kwa Nchi za Afrika?
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania kwa kushirikiana na Nchi za Kenya na Uganda imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya Mataifa ya Afrika Mwaka 2027 (AFCON 2027); ambapo kupitia mashindano haya fursa mbalimbali zitapatikana zikiwemo ajira kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo itakayotumika wakati wa mashindano hayo, uuzaji wa vifaa vya ujenzi, kuongezeka kwa mapato katika biashara mbalimbali kutokana na matumizi kwa wageni na wadau watakaoingia nchini kushuhudia mashindano, kuongezeka kwa mapato katika huduma za jamii kama vile hoteli, nyumba za kulala wageni, migahawa, usafirishaji na huduma nyingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, fainali hizi pia ni fursa kwa wachezaji wa Kitanzania kuonyesha vipaji vyao kwa mawakala wa vilabu vya kimataifa. Aidha, mashindano haya yatawezesha vikundi vya sanaa na utamaduni kujitangaza hivyo kutangaza utamaduni wa Tanzania.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved