Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 125 2025-02-05

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: -

Je, upi mkakati wa Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa utoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya wanyama?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imetengeneza Kanuni ya Chanjo na Uchanjaji ambayo ilitolewa kupitia GN 180 ya Mwaka 2020. Aidha, katika kanuni hii inaelekeza kuwa uchanjaji wa mifugo ni wa lazima (compulsory vaccination). Vilevile, Serikali imeendelea kutoa elimu kwa umma ikiwemo kufanya uzinduzi wa uhamasishaji wa Kampeni ya Chanjo Kitaifa ambayo ilifanyika tarehe 18 -19 Desemba, 2024.

Mheshimiwa Naibu Spika, uzinduzi huo ni sehemu ya mkakati ambayo ililenga kutoa elimu kwa wataalam kutoka Mamlaka ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Viongozi wa Vyama vya Wafugaji, Viongozi wa Vyama vya Kitaaluma na Wafugaji kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Kampeni ya Chanjo Kitaifa. Aidha, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia makundi hayo itaendelea kuhamasisha kampeni hii na kutoa elimu nchi nzima. Ahsante