Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, upi mkakati wa Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa utoaji chanjo dhidi ya magonjwa ya wanyama?

Supplementary Question 1

MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa elimu ya chanjo ili kudhibiti utumiaji holela au kupunguza utumiaji wa anti-biotic?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanyama wanaozurura kama mbwa na paka hasa kwenye migahawa. Je, Serikali ina mkakati gani wa kudhibiti ongezeko hilo maana ni rahisi wanyama hawa kuwa na ugonjwa wa kimeta au rabies ambao unaweza kusababisha magonjwa na hatari kwa binadamu?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na hili la kwanza juu ya matumizi ya antibiotic; tayari Serikali imeshatoa maelekezo mbalimbali kupitia Maafisa Ugani wanaopatikana katika maeneo mbalimbali katika vijiji vyetu. Sasa hivi cha kwanza kabisa ambacho tunakifanya ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya anti-biotic zinazopatikana katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wafugaji popote walipo wanafahamu namna sahihi ya matumizi ya anti-biotic na wale ambao hawana huo ufahamu basi tumekuwa tukiwaelimisha na kuwaelekeza mahali sahihi; kwenda kujifunza kwa Maafisa Ugani ili waweze kutumia anti-biotic kwa mujibu wa utaratibu unaotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii siyo tu kwa mifugo bali pia kwa binadamu. Kwamba huwezi kutumia antibiotic ama dawa yoyote ambapo daktari wa mifugo au wa binadamu bado hajathibitisha matumizi hayo. Tunaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wafugaji wote kwenda kwa Maafisa Ugani ili waweze kupata utaratibu unaotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hili la pili, anachosema Mheshimiwa Mbunge ni kweli, baadhi ya maeneo hasa maeneo ya Kaskazini ongezeko la mifugo kama mbwa limekuwa kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba Serikali tumeshatoa maelekezo kwa Maafisa Ugani na Serikali katika maeneo hayo kuchukua hatua dhidi ya mifugo yote isiyokuwa na wenyewe, hasa aina ya mbwa; mbwa akizurura mtaani kwako na hana mwenyewe na Serikali za mitaa zikajiridhisha kwamba mbwa huyu hana pa kwenda na pengine ameshapata maambukizi ya kichaa cha mbwa, hatua stahiki ambazo tumekwishawaelekeza ni pamoja na kuwaondoa Duniani ili mbwa hao wasilete madhara kwa binadamu, nakushukuru.