Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 7 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 126 2025-02-05

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kununua magari ya Zimamoto kwa ajili ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji inatekeleza mradi wa ununuzi wa magari 150 pamoja na vifaa mbalimbali vya kuzima moto na uokoaji wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 100 kutoka kampuni ya NAFFCO FZCO (National Fire Fighting Manufacturing Company Free Zone Company) iliyopo Dubai. Pindi magari yatakapowasili nchini, yatasambazwa nchi nzima ikiwemo wilaya za Mkoa wa Simiyu. Ahsante.