Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kununua magari ya Zimamoto kwa ajili ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu?

Supplementary Question 1

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kwa kuwa majibu yake ya msingi amesema magari hayo yatasambazwa nchini kote, tunataka kujua ni lini hasa magari hayo yatasambazwa, ikiwemo Mkoa wa Mtwara na Wilaya zake Masasi, Newala, Nanyumbu na Tandahimba?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Hokororo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, magari haya yatawasili hapa nchini kwa awamu nne, awamu ya kwanza itaanza mwezi Aprili mwaka huu na kuendelea. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba magari haya yatasambaa maeneo yote aliyoyataja ikiwemo pia Mkoa wa Mtwara. Ahsante.