Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 215 2025-02-13

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:-

Je, asilimia ngani ya waajiri nchini wamejiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na unawanufaishaje?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Benardeta Kasabago Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Desemba 2024, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umesajili 93.39% ya waajiri wote kutoka katika mikoa yote Tanzania Bara waliotambuliwa na mfuko. Manufaa ya WCF kwa waajiri ni kuwa mwajiri anapojisajili na mfuko anaondokana na wajibu wa kuwapatia wafanyakazi wake huduma za matibabu au kuwalipa fidia pale wanapopata madhila na wanapoumia au kupata ajali, magonjwa ama kifo wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao. Jukumu hilo linabebwa na mfuko kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263. Ahsante.