Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, asilimia ngani ya waajiri nchini wamejiunga na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na unawanufaishaje?

Supplementary Question 1

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kwenye majibu yake ya msingi amezungumzia juu ya fidia, ningependa atueleze kinagaubaga, huo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unatoa mafao gani hasa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa WCF ni mfuko ambao unatoa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia au kufariki kabisa wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi, lakini kwa kuwa mfuko huu unachangiwa na mwajiri tu, je, yule mwajiri ambaye anashindwa kujisajili kwenye WCF na hivyo kuwafanya wafanyakazi wake wakakosa mafao haya anachukuliwa hatua gani?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mushashu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni mfuko maalumu ulionzishwa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyakazi wanapopata madhila yanayotokana na kazi kwenye maeneo yao na hivyo inapotokea aidha mfanyakazi ameugua na ugonjwa huo umesababishwa na eneo lake la kazi ama amepata ajali itakayoathiri afya yake au viungo vyake mfuko unachukua jukumu moja kwa moja la kuweza kufanya huduma zote za matibabu, lakini pia kutoa gharama za utengamao kuweza kuhakikisha anakuwa salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikitokea kifo hivyo hivyo mfuko unachukua jukumu hilo kwa niaba ya mwajiri ambaye tayari atakuwa amesajiliwa na kwamba alikuwa analipa zile tozo ambazo zimeelekezwa na sheria. Hii ni pamoja na changamoto nyingine zozote ambazo anazipata na magonjwa kama igonomia yanayotokana na kazi. Kwa hiyo mfuko unabeba jukumu hilo na unamsaidia mwajiri kuweza ku-deal na mambo ya uzalishaji zaidi na uwekezaji kuliko kushughulika na mfanyakazi mmoja mmoja ambapo mfuko unabeba jukumu hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, faida zake zipo nyingi kwa mujibu wa sheria, lakini kwa sababu ya muda nieleze kwa ufupi hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili waajiri wanachukuliwa hatua gani ikiwa hawajajisajili. Utaratibu wa usajili ni jukumu kwanza la mwajiri ndiye anayepaswa kujisajili. Pia mfuko tunachukua jukumu hilo la kuweza kuhakikisha tunawatafuta. Mpaka sasa tumeshaenda maeneo ya kazi zaidi ya 37,726 ambayo haya ni maeneo ya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tofauti yake hapa, jinsi WCF inavyofanya kazi kuna tofauti na taasisi nyingine zinazosajili maeneo ya kazi. Mathalani tukichukulia benki moja ya NMB au CRDB; CRDB ina branches 90 na katika hizi branches 90 kwa mwingine angeweza kusajili kama ni maeneo ya kazi 90 au waajiri 90, lakini kwa WCF huyo ni mwajiri mmoja. Tunafanya kazi hiyo na tunaendelea kukaribia kufikia target, tupo zaidi ya 93% kati ya waajiri 40,000 ambao tunatarajia kuweza kuwapata.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutaendelea kuchukua hatua kwa wale ambao hawataona umuhimu wa kujisajili na sisi kama mfuko bado tunaendelea kuchukua jukumu la kutoa elimu na kuwatembelea kwenye maeneo yao.