Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 216 2025-02-13

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: -

Je, lini Mradi wa TACTIC Tire II utaanza na ni lini unatarajiwa kukamilika kwenye manispaa zinazohusika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, usanifu wa Mradi wa TACTIC katika kundi la pili ambao unajumuisha miji 15 ikiwemo Manispaa ya Moshi tayari umekamilika na nyaraka za zabuni kuwapata wakandarasi na wasimamizi ziliandaliwa na kutangazwa kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Umma (NeST) mapema wiki hii. Aidha, utekelezaji wa ujenzi unatarajiwa kuanza ifikapo Mei, 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha miji katika Mikoa na Wilaya zake kwa ajili ya kujenga miundombinu muhimu ili kupendezesha miji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, ahsante.