Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: - Je, lini Mradi wa TACTIC Tire II utaanza na ni lini unatarajiwa kukamilika kwenye manispaa zinazohusika?

Supplementary Question 1

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na nikiri nimeshaliona tangazo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa sababu tulishawahi kuleta hapa maombi ya kuombea wakandarasi wazawa waweze kupewa hii miradi ya Benki ya Dunia na Serikali iliridhia, Mheshimiwa Waziri anaweza kutuhakikishia kwamba wakandarasi wazawa watapewa kazi kwenye miradi hii? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa mfano, kwa sababu kwenye barabara kunakuwa na barabara nyingi, Serikali iko tayari kuweka wakandarasi zaidi ya mmoja ili kazi iweze kukamilika mapema?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, ni kweli kwamba Serikali iliweka mpango wa kuwahusisha kwa karibu wakandarasi wazawa katika kutekeleza miradi hii ya TACTIC na nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge mpango wa Serikali ni kuendelea kuwapa kipaumbele wazawa, wale ambao watakidhi vigezo na kuwa na ushindani kulingana na taratibu za manunuzi ya Serikali. Kwa hiyo, wale ambao watakuwa na sifa hizo na watakuwa na vigezo na watashinda zabuni hizo, watapata miradi hiyo. Pia nitumie nafasi hii kuendelea kuwahamasisha wakandarasi wa ndani kutumia fursa hizi mara zinapotangazwa ili waweze kupata miradi hiyo na kuitekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili; barabara ambazo ziko kwenye Mradi wa TACTIC ziko za urefu tofauti tofauti, lakini Serikali imeweka utaratibu wa kupata makandarasi kuzijenga barabara hizo. Hata hivyo, tunapokea wazo lake, tutalifanyia tathmini na kuona ikiwa barabara ni ndefu sana na inahitaji muda mfupi zaidi kutekeleza tutaona namna ya kuboresha ili utekelezaji wake uweze kukamilika kwa wakati, ahsante.

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: - Je, lini Mradi wa TACTIC Tire II utaanza na ni lini unatarajiwa kukamilika kwenye manispaa zinazohusika?

Supplementary Question 2


MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara za Mradi wa World Bank ambao unatekelezwa Dar es Salaam, Mradi wa DMDP wakandarasi wameshapatikana, je, wakandarasi hawa wataanza ujenzi lini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu Dar es Salaam (DMDP) uko kwa awamu au makundi tofauti. Kuna kundi la kwanza, kundi la pili, lakini kwa kundi la pili ni kweli makandarsi wameshapatikana na tunatarajia wakati wowote kuanzia sasa watasaini mikataba kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo katika maeneo mbalimbali ambayo yamekwishatangazwa, ahsante.

Name

Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: - Je, lini Mradi wa TACTIC Tire II utaanza na ni lini unatarajiwa kukamilika kwenye manispaa zinazohusika?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Mheshimiwa Waziri, Halmashauri ya Korogwe TC pia ina mradi wa TACTIC. Wananchi wamekwisha pisha ujenzi wa mradi huo, je, unawaahidi kwamba lini wakandarasi wataonekana kwenye Halmashauri ya Korogwe Mji wakianza kazi ya kutengeneza barabara hizo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, Halmashauri ya Korogwe Mji iko kwenye mpango wa utekelezaji wa Miradi ya Uboreshaji wa Miji 45 (TACTIC). Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Korogwe Mji kwamba Serikali iko kwenye hatua mbalimbali za ununuzi na mara hatua hizo zitakapokamilika makandarasi watakwenda kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kutekeleza miradi yote iliyomo kwenye package ya Korogwe Mji, ahsante.