Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Good Governance Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 217 2025-02-13

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: -

Je, wananchi watarajie nini baada ya kumalizika kwa Mradi wa TASAF?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo kwenye maandalizi ya kuendelea na Kipindi cha Tatu cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambacho utekelezaji wake utakuwa wa miaka mitano kuanzia mwaka 2026 hadi mwaka 2030 katika maeneo yote ya Tanzania. Lengo la Kipindi cha Tatu cha Mpango ni kuendelea kupambana na umaskini wa kaya za walengwa zenye hali duni ikiwa ni pamoja na makundi maalumu ya watoto na wazee. Mpango unalenga kuzijengea kaya hizi ujuzi wa ujasiriamali ili waweze kuwa na misingi ya kujitegemea. Mpango huu utaendelea kutumia dhana ya ushirikishwaji jamii ili kufikia malengo ya kupambana na umaskini, nashukuru.