Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 218 2025-02-13

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kurudisha bei ya shilingi 27,000 kuunganisha umeme kwa wananchi walioshindwa kulipia shilingi 320,000?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za kuunganisha umeme zinafuata mwongozo uliowekwa na Serikali ambapo kwa maeneo ya vijijini, gharama ni shilingi 27,000 na nje ya hapo ni shilingi 320,960. Katika kuhakikisha tunapunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi, Serikali inatekeleza miradi ya kusogeza huduma ya umeme karibu na wananchi ikiwemo Miradi ya Peri-Urban kwa maeneo ya miji na miradi ya kupeleka umeme vitongojini kwa maeneo ya vijijini, ahsante.