Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Juma Makoa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kondoa Mjini
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurudisha bei ya shilingi 27,000 kuunganisha umeme kwa wananchi walioshindwa kulipia shilingi 320,000?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana na pamoja na hayo ninampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya katika jimbo ikiwemo kuwapelekea wananchi wetu umeme. Pia ninawapongeza Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya katika jimbo langu. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mitaa minne ambayo haijapata umeme. Sasa kuna mitaa mitatu ya Mongoroma, Chandimu na Hachwi hawajapata umeme kabisa. Nini mpango wa Serikali wa kufanya haraka na hawa pia wapate umeme?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, iko Mitaa ya Tampori, Kwa Mtwara pamoja na Chemchem wamepata Mradi wa REA lakini TANESCO wamekosa nguvu ya kufikisha umeme mkubwa kwenye haya maeneo na wameshindwa nguvu kidogo tu.
Je, Serikali iko tayari siku mbili, tatu hizi ikawapelekea japo nguzo 200 ili TANESCO waweze kufikisha ule umeme, REA wanasambaza wananchi waendelee kupata huduma?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nishukuru kwa maswali mazuri ya Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ilikuwa mitaa sita katika Jimbo la Kondoa Mjini ambayo ilikuwa na changamoto ya umeme na kupitia mradi wetu wa kupeleka umeme vijijini, mitaa mitatu ilipata mradi na mitaa mitatu ya Mongoroma, Chandimu na Hachwi bado haijapata mradi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, nia ya Serikali ni kuhakikisha maeneo haya yanapata umeme na kwa yale maeneo ya Tampori, Chemchem na Kwa Mtwara ambayo yanahitaji nguzo takribani 188, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri nimeshamwelekeza meneja pamoja na makao makuu watafute angalau nguzo 100 ili tuweze kuanza katika mitaa hii mitatu. Ile mitaa mingine mitatu tunafanya mikakati kuhakikisha kwamba tunapeleka umeme mkubwa na wananchi wanaendelea kupata umeme wa uhakika, ahsante sana.
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurudisha bei ya shilingi 27,000 kuunganisha umeme kwa wananchi walioshindwa kulipia shilingi 320,000?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Mji wa Iguguno haujawahi kuwa mji, lakini mpaka sasa wanapelekewa umeme kwa shilingi 320,000. Lini Serikali itatoa tamko ili wananchi wa Iguguno waache kuteseka? (Makofi)
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, namna ambayo maeneo yanatozwa kwa kadiri ya mwongozo ambao tunao, tumeweka maeneo haya kwa maana ya miji pamoja na vijiji miji pamoja na maeneo ya vijijini. Kwa hiyo, kwa yale maeneo ambayo ni vijiji miji na maeneo, lakini ambayo ni miji gharama yake ni hiyo shilingi 320,960 na yale maeneo ambayo yamekuwa categorized kama vijiji gharama yake ni shilingi 27,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye eneo analolisema Mheshimiwa Mbunge, tutaenda kufanya mapitio tuonea kama vile vigezo ambavyo vimewekwa havikidhi eneo hilo kuwa-charged shilingi 320,960 na baada ya hapo tutakuja na majibu ya mwisho, ahsante.
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurudisha bei ya shilingi 27,000 kuunganisha umeme kwa wananchi walioshindwa kulipia shilingi 320,000?
Supplementary Question 3
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaipongeza sana Serikali kwa kupeleka umeme kwenye vijiji vyote Mkoa wa Mbeya, baadhi ya vitongoji havijafikiwa na umeme kwenye Wilaya ya Rungwe, Kyela, Busokelo, Mbarali, Mbeya Jiji, Mbeya Vijijini na Chunya. Je, ni lini Serikali itampeleka mkandarasi ili aweze kuanza kupeleka umeme kwenye hivyo vitongoji? Ahsante.
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mkoa wa Mbeya mkandarasi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 alikuwa amechelewa, lakini nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba mkandarasi yupo katika hatua za mwisho za kupatikana na hivi karibuni atapatikana na tutaanza kazi ya kupeleka umeme kwenye hivi vitongoji 15 vya kila jimbo. Vilevile tunao mradi mkubwa kwa mwaka huu wa fedha kupeleka umeme kwenye vitongoji takribani 8,000. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, majimbo haya yote ambayo ameyataja na yenyewe yatanufaika na mradi huu ambao hivi karibuni tutautangaza, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved