Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 13 | Industries and Trade | Wizara ya Viwanda na Biashara | 219 | 2025-02-13 |
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:-
Je, lini Serikali itatafuta wawekezaji wa viwanda vidogovidogo vya kuongeza thamani katika zao la ndizi?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru, mkakati wa Serikali wa kutafuta wawekezaji wa viwanda vidogo ni kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI) kwa kuwajengea uwezo Watanzania ili waanzishe viwanda vidogo. Sambamba na hilo, pia Serikali imeendelea kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vikubwa vya kuchakata mazao ili kuyaongezea thamani kwa wingi zaidi ikiwemo zao la ndizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) imeendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo katika maeneo yao kulingana na fursa zinazopatikana huko ili waweze kufanya uwekezaji wa viwanda vidogo vya kuchakata mazao mbalimbali ikiwemo zao la ndizi kwa kuwezesha teknolojia za usindikaji wa kaukau za ndizi, mvinyo wa ndizi, pombe kali na unga wa ndizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved