Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Water and Irrigation Wizara ya Maji 221 2025-02-13

Name

Soud Mohammed Jumah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Donge

Primary Question

MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH aliuliza:-

Je, Serikali ina mikakati gani ya kuvilinda na kuvihifadhi vyanzo vya maji nchini kwa kuzihusisha sekta za misitu, kilimo na mifugo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maji inaendelea na programu maalumu ya uhifadhi wa vyanzo vya maji iliyoanza mwaka 2021 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2035. Utekelezaji wa programu hiyo unashirikisha sekta zinazohusiana na maji pamoja na taasisi zake ambapo utekelezaji wake unafanyika kupitia Timu ya Kisekta ya Kitaifa iliyoundwa kwa kujumuisha sekta za Maji, Kilimo, Mifugo, Maliasili na Mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia programu hiyo kazi mbalimbali za uhifadhi wa vyanzo vya maji zinatekelezwa ikiwemo kutambua vyanzo vya maji, kuweka mipaka na kuvitangaza vyanzo hivyo kwenye Gazeti la Serikali, kupanda miti rafiki kwa maji katika vyanzo vya maji na kufanya kilimo na ufugaji rafiki wa mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa jumla ya vyanzo 3,285 vimetambuliwa ambapo kati ya hivyo 327 vimewekewa mipaka na vyanzo 68 vimetangazwa katika Gazeti la Serikali kuwa maeneo tengefu. Aidha, jumla ya miti rafiki 5,381,548 imepandwa katika vyanzo maji mbalimbali nchini. Ahsante sana.