Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 222 2025-02-13

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja ya kukipatia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Tawi la Tunduru eneo la kiwanda cha kubangua korosho kilichotelekezwa?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya kulifanya eneo la kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma kama Tawi la SUA ni la muhimu na Serikali imepokea. Aidha, Serikali itakaa pamoja (Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na mmiliki wa kiwanda ambaye ni Wizara ya Viwanda na Biashara) ili kufanya mazungumzo na tathmini kabla ya maamuzi ya SUA kulichukua eneo hilo.