Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, Serikali haioni haja ya kukipatia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Tawi la Tunduru eneo la kiwanda cha kubangua korosho kilichotelekezwa?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri yanayoleta matumaini. Nina mawili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, je, mpaka sasa ni programu gani zinaendelea pale SUA?

Swali la pili, ni lini Waziri sasa ataamua kupeleka Kamati ya Elimu, Tunduru ili ikaone kazi zinazofanyika pale? Ahsante.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na jambo lake la kwanza ambalo linazungumzia suala la programu gani, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyokwishakueleza kwenye majibu ya swali la msingi, eneo hili la Tunduru kwa hivi sasa linatumika na Chuo chetu cha SUA kwa lengo la kutoa yale mafunzo ya vitendo kwa kozi za sayansi ya misitu na usimamizi wa wanyamapori kwa wale wanafunzi wa shahada ya kwanza ambao wanasoma kwa kipindi cha miaka mitatu pale chuoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninafahamu kwamba dhamira ya Dkt. Thea ni kulifanya eneo hili kuwa campus ya Chuo Kikuu cha SUA. Nimuondoe hofu, kwa hivi sasa lile eneo ni dogo, lina ukubwa wa ekari tisa na hivi sasa tuko kwenye mazungumzo Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ili kutuongezea eneo la angalau ekari 300 ili tuweze kufungua campus kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili anazungumzia kuhusu Kamati yetu ya Bunge, kwamba ni lini inaweza kwenda?

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tutakaa na Mwenyekiti wa Kamati na sisi kama Wizara tuweze kupanga ratiba vizuri ili ikiwezekana kabla ya Bunge la mwezi wa nne, tuweze kutembelea eneo hili la Tunduru ili na ninyi wenyewe mkajionee maendeleo yaliyofanywa na Chuo chetu cha SUA. Nakushukuru sana.