Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 13 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 223 2025-02-13

Name

Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza:-

Je, lini Jeshi la Zimamoto Korogwe TC litapatiwa gari jipya la zimamoto?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe lipo gari moja la zimamoto na uokoaji aina ya Isuzu lenye ujazo wa lita 5000 za maji linalotumika kwa shughuli za maokozi. Kwa sasa Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji inatekeleza mradi wa ununuzi wa vifaa na magari ya kuzima moto na uokoaji wenye thamani ya dola za Marekani milioni 100 kutoka kwa Kampuni ya NAFFCO FZCO iliyopo Dubai. Mradi huo utawezesha kupatikana kwa vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari 150 ya kuzima moto na uokoaji yatakayosambazwa nchi nzima ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ahsante.