Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza:- Je, lini Jeshi la Zimamoto Korogwe TC litapatiwa gari jipya la zimamoto?

Supplementary Question 1

MHE. DKT ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ambayo Serikali imejibu, hata hivyo, nataka kutoa msisitizo kwamba gari lililopo mara nyingi linaharibika sana na Mji wa Korogwe ni mji unaokuwa kwa kasi, majanga ya moto yanatokea mara nyingi na tunashindwa kuya-control.

Je, Serikali inatuhakikishia ni lini magari hayo yatapatikana ili Mji wa Korogwe upate gari jipya na zuri ili tuachane na hili la zamani? Ahsante sana.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kimea kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, mradi huu tayari tumeshaagiza magari na tumeyalipia. Kwa hiyo, Mbunge awe na subira, magari yatafika na Mji wa Korogwe utapata gari kwa ajili ya zimamoto na uokoaji, ahsante.

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza:- Je, lini Jeshi la Zimamoto Korogwe TC litapatiwa gari jipya la zimamoto?

Supplementary Question 2

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, katika Jimbo la Tarime Vijijini, tarehe 8 kuamkia tarehe 9 walitekwa watu watatu akiwepo Mwenyekiti wangu wa Chama Cha Mapinduzi, Kata ya Itiro. Mpaka leo asubuhi hakuna taarifa yoyote ambayo imetolewa na RPC, OCD wala DC, badala yake wanasema hawajui hao watu wako wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hilo limekuwa linazua taharuki, watu wamekuwa wakipigiwa simu za vitisho na maswali yao wanauliza ya kisiasa sana.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara, swali lako? Uliza swali.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ningeomba sasa Wizara ya Mambo ya Ndani, itoe kauli juu ya jambo hilo la utekaji na hali tete iliyopo kule Itiro, ili wananchi wengi waendelee kuishi kwa amani? Ahsante.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea taarifa, saa saba nitalifanyia kazi na tutaongea na Mheshimiwa Mbunge tujue tunafanyaje…

NAIBU SPIKA: Kwa hiyo, kaa naye ulifanyie kazi.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.