Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 12 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 196 | 2025-02-12 |
Name
Aleksia Asia Kamguna
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Watumishi na Vifaa Tiba katika Vituo vya Afya vya Kasanga, Kisemo na Kisaki Morogoro Vijijini?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 na 2024/2025, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imepokea jumla ya shilingi bilioni 1.65 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaatiba. Kiasi cha shilingi milioni 266 kimetumika kununua vifaatiba katika Kituo cha Afya Kasanga shilingi milioni 43, Kituo cha Afya Kisemo shilingi milioni 13 na Kituo cha Afya Kisaki shilingi milioni 210. Aidha, shilingi bilioni 1.4 zilipelekwa katika hospitali ya wilaya na vituo vingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuajiri wataalam wa kada za afya, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024, Serikali imeajiri jumla ya watumishi 25,917 wa kada za afya kote nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilipangiwa jumla ya wataalam wa kada za afya 1,108 ambao wamepelekwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya vikiwemo Vituo vya Afya vya Kasanga, Kisemo na Kisaki.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved