Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 12 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 197 | 2025-02-12 |
Name
Sylivia Francis Sigula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza:-
Je, lini Serikali itarejesha mikopo ya 10% iliyokuwa ikitolewa kwa Vijana, Wanawake na Watu Wenye Ulemavu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inayotolewa kutokana na 10% ya mapato ya ndani ya halmashauri, ilisitishwa na Serikali tarehe 13 Aprili, 2023 ili kupisha maandalizi ya utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo hiyo. Kufuatia kukamilika kwa mfumo mpya wa utoaji wa mikopo, Serikali ilitangaza tarehe Mosi Julai, 2024 mikopo hiyo itaanza kutolewa tena kwa mujibu wa sheria na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inaendelea kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinatoa mikopo kwa mujibu wa sheria, ambapo tangu mikopo kurejeshwa hadi Disemba, 2024, halmashauri 64 zimetoa mikopo ya shilingi bilioni 22.07. Kati ya hizo shilingi bilioni 27.76 ziliombwa na vikundi 2,726 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kati ya fedha hizo shilingi billioni 21.88 zimetolewa kutokana na michango ya Halmashauri (10% ya mapato ya ndani) na shilingi milioni 194.3 ni mikopo iliyotokana na fedha za marejesho.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved