Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 198 2025-02-12

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG'WASI D. KAMANI aliuliza:-

Je, upi mkakati wa kuendelea kuwezesha upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa Makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inatolewa kutokana na 10% ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa mujibu wa kifungu 37A cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu za mwaka 2024.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuboresha na kuhakikisha mfumo wa kutolea mikopo isiyo na riba kwa makundi haya ikiwa ni pamoja na maboresho ya sheria na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo ya 10% ya mwaka 2024; pamoja na kuimarisha mfumo wa kielektroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo ili kuongeza ufanisi katika utambuzi wa walengwa, usimamizi wa mikopo na urejeshaji wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na makundi haya ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kunufaika na mikopo ya 10% isiyo na riba, bado wanaweza kunufaika na mikopo yenye riba nafuu katika taasisi za fedha zilizopo nchini.