Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 199 2025-02-12

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itasajili na kutangaza rasmi barabara mpya ili kuongeza Mtandao wa Barabara za Mkoa wa Tanga zilizo chini ya TARURA?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Tanga umekamilisha taratibu za ndani za kujadili na kupitisha maombi ya kupandishwa hadhi/kusajiliwa barabara ambazo hazikuwa katika mtandao wa barabara za TARURA. Maombi hayo tayari yamewasilishwa Wizara ya Ujenzi kwa ajili ya taratibu zaidi.