Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwanaisha Ng'anzi Ulenge
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:- Je, lini Serikali itasajili na kutangaza rasmi barabara mpya ili kuongeza Mtandao wa Barabara za Mkoa wa Tanga zilizo chini ya TARURA?
Supplementary Question 1
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa mujibu wa Sheria ya Barabara ya Mwaka 2007 sehemu ya tatu, kifungu cha 11(1) ambacho kinampa mamlaka Waziri wa Ujenzi kuweza kuzipandisha hadhi au kuzishusha hadhi; na kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema ameshapeleka Wizara ya Ujenzi, ninaomba sasa tumsikilize kwa ridhaa ya kiti chako, Waziri wa Ujenzi kama wameweza kupokea hayo ili niweze kuuliza maswali ya nyongeza. Ahsante sana.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mwanaisha Ulenge kwa maoni yake. Sisi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI, tutaendelea kufanya mawasiliano kwa karibu kabisa na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi ambao kwa mujibu wa Sheria ya Barabara (The Road Act) ya mwaka 2007, Wizara ya Ujenzi wamepewa mamlaka ya upandishaji wa hizi barabara. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kufanya uratibu na mawasiliano ndani ya Serikali ili kuweza kufuatilia kwa ukaribu upandishaji wa barabara hizi ambazo maombi yake wao kama Mkoa wa Tanga wameshawasilisha.
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:- Je, lini Serikali itasajili na kutangaza rasmi barabara mpya ili kuongeza Mtandao wa Barabara za Mkoa wa Tanga zilizo chini ya TARURA?
Supplementary Question 2
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi. Barabara za Barikiwa - Mkutano, Nabuu ya Tepetepe, Mlembwe- Barikiwa, Mkutano - Kimambi na Makinda - Ngorongopa zote hizi tumeshaziombea ili ziweze kusajiliwa kuongeza mtandao wa barabara kwenye Halmashauri yetu ya Liwale. Je, ni lini Serikali itatusajilia hizo barabara?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Kuchauka kwa swali lenye maslahi mapana ya kuhakikisha wananchi wake wanapata barabara ambazo zinahudumiwa na TARURA. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi kama Serikali kwa pamoja tutafanya mawasiliano ya ndani ili kuweza kupata muafaka wa maombi yao haya ya kuzitambua barabara hizi alizozitaja na kuziingiza katika mtandao unaohudumiwa na TANROADS.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved