Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 200 2025-02-12

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kujenga Madaraja ya Chikundi katika Wilaya ya Masasi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kujenga madaraja mbalimbali yaliyo katika Kata ya Chikundi, Wilayani Masasi, ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024, Daraja la Nasindi lilitengewa shilingi milioni 13.7 kwa ajili ya kukarabati nguzo ya daraja. Kazi hiyo bado inaendelea kutekelezwa na mkandarasi yuko eneo la kazi. Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga milioni 16.833 kwa ajili ya kuweka kifusi cha changarawe kilomita moja katika Barabara ya Mbaju – Litamwa kwenye maingilio ya daraja ambapo tayari kazi hii imeshaanza kutekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali imeweka katika mipango yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026, shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuweka kifusi kilomita moja kwenye maingilio ya Daraja la Lukuledi katika Barabara ya Mtunungu – Lukuledi. Serikali inaendelea kuihudumia miundombinu ya Barabara ya Wilaya ya Masasi ikiwemo ujenzi wa madaraja kulingana na upatikanaji wa fedha.